ISHA MASHAUZI AACHIA NGOMA MPYA YA ZOUK RUMBA “JIAMINI”
Mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi, amezidi kudhihirisha kuwa yuko vizuri hata nje ya taarab baada ya kuachia ngoma yake mpya “JIAMINI” iliyoko katika miondoko ya zouk rumba.
Unaambiwa ngoma hiyo iliyofanywa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitchou Mechant, imetiwa mkono na mkali wa kinanda Fred Manzaka kutoka Mashujaa Band na mchawi wa bass Dekanto wa Akudo Impact huku solo gitaa likikung’utwa na Pitchou ambaye pia anaitumikia Akudo Impact.
Sauti zote utakazozikia kwenye wimbo huu wa dakika nne, ni za kwake Isha Mashauzi.
Hii inakuwa ngoma ya nne ya Isha Mashauzi nje ya taarab baada ya “Nimlamu Nani”, “Nimpe Nani” na “Usisahau”
0 comments:
Post a Comment